Kiswahili kuwa lugha rasmi nchini Rwanda
Lugha ya Kiswahili imeongezwa kwenye orodha ya lugha rasmi
zinazokubaliwa na serikali ya Rwanda, baada ya Kinyarwanda, Kiingereza na
Kifaransa.
Uamuzi huo umetolewa na baraza la mawaziri lililokusanyika Jumanne tarehe 12
Oktoba mwaka huu.
Katiba ya Rwanda iliyorekebishwa mwaka jana, ilitaja lugha
tatu zinazokubaliwa kutumiwa katika mambo ya uongozi.
Lakini katiba hiyo iliachia uwezekano wa kuongeza au kuondoa
lugha moja kati ya hizo.
Kiswahili kilikuwa kikifundishwa shuleni kuanzia shule za
sekondari.
Katika mtaala mpya wa masomo uliozindua na Wizara ya elimu mwaka
huu, Kiswahili kitafundishwa hata shule za msingi, na kitaulizwa katika
mitihani ya taifa.
Rwanda inaunga mkono nchi kama Uganda na nyinginezo zinazounda
Jumuia ya Afrika ya Mashariki zinazo Kiswahili kama lugha rasmi.
No comments: